info@chadema.or.tz Daima Street, Mikocheni, Dar Es Salaam

LISSU APATA MARADHI GEREZANI

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mheshimiwa Tundu Lissu anaumwa maumivu makali ya tumbo.

Akiutangazia umma jana Jumapili Mei, 17, 2026 Makamu Mwenyekiti Bara, Mheshimiwa John Heche amesema alipigiwa simu na mdogo wa Lissu akimueleza kuwa Mwenyekiti ana maumivu makali ya tumbo.

Mheshimiwa Heche ameitaka mamlaka kumuachia Lissu kwani lolote baya likimtokea, Watanzania hawatakubali.

Mheshimiwa Lissu ambaye yupo gerezani kwa kesi ya uongo ya uhaini tangu Aprili 9, 2025 alikuwa anaendelea na matibabu ambapo kila mwezi alikuwa anasafiri kwenda nje ya nchi kupata matibabu. Tangu awekwe gerezani hajapata huduma hiyo ya matibabu.

Mheshimiwa Heche na viongozi wengine wa chama wapo kwenye operesheni ya mikutano ya hadhara ya kudai katiba mpya na Lissu aachiwe.

Leo operesheni hiyo itafanyika Kahama ambapo mkutano wa hadhara utaanza saa nane mchana.

Leave A Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *