Katibu Mkuu wa Chadema, Mheshimiwa John Mnyika amewaongoza wananchi wa Kahama kumtaka Jaji Mkuu kupanga usikilizwaji wa kesi ya Mwenyekiti Tundu Lissu iliyokwama kusikilizwa tangu Februari mwaka huu.
Mheshimiwa Mnyika amesema kutoipangia tarehe ya kuisikiliza kesi hiyo iliyopo mahakama ya rufaa ni kuchelewesha haki kwa Mwenyekiti aliyepo gerezani kwa miezi 13 sasa.
“Serikali imepaki basi kuendelea kuisikiliza rufaa iliyokatwa kwenye mahakama ya rufaa tangu Februari. Wananchi wa Kahama kwa pamoja kwanza tumtake Samia na DPP waifute kesi hiyo kwani haina maslahi na jamhuri,” alisema Mnyika
Kesi hiyo ya uhaini imekwama mahakama ya rufaa baada ya mawakili wa jamhuri kuyakatia rufaa maamuzi madogo yaliyotolewa mahakama kuu.
Ili kesi hiyo iendelee ni lazima jaji mkuu apange tarehe ya kusikiliza rufaa hiyo kabla ya kuirudisha mahakama kuu ili usikilizwaji wa kesi ya msingi ya uhaini uendelee.
Jumuiya ya kimataifa ikiwemo bunge la Ulaya, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na taasisi mbalimbali za haki za binadamu wamesema kesi ya uhaini aliyofunguliwa Mwenyekiti Lissu ni ya Kisiasa na inapaswa kufutwa
© Copyright 2025. Developed By: CHADEMA
Leave A Reply