Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Mheshimiwa Saidi Mzee Saidi amesema kadi mpya namba tatu ya Chadema haijatolewa kwa mtu yoyote.
Kauli hiyo ameitoa jana Jumatatu, Mei 18, 2026 wakati akihutubia mkutano wa hadhara Kahama mkoani Shinyanga.
Mhe. Mzee amesema kadi hiyo ni maalum kwa marehemu Bob Makani mzaliwa wa Kahama ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Chadema kilipoanzishwa mwaka 1992.
Mheshimiwa Mzee amewataka wakazi wa Kahama kuilinda Chadema kama alivyoilinda marehemu Makani kwa muda wote wa maisha yake.
Mheshimiwa Mzee na viongozi wengine wakuu wa chama wapo kwenye operesheni ya mikutano ya hadhara ya kudai Katiba Mpya na kutaka mwenyekiti Lissu aachiwe huru.
Baada ya Kahama, mkutano unaofuata ni wa Mei 22 utakaofanyika mkoani Arusha Mjini kwenye kiwanja cha Relini.
© Copyright 2025. Developed By: CHADEMA
Leave A Reply