Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa salamu za pole za dhati kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao, pamoja na wote walioguswa na ajali ya kusikitisha ya barabarani iliyotokea usiku wa tarehe 07 Juni 2025 katika eneo la Mlima Iwambi, mkoani Mbeya, ambapo watu 28 wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa.
Tunatambua majonzi, huzuni na mshtuko mkubwa mlionao katika kipindi hiki kigumu. Tunawaombea faraja, subira na nguvu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili muweze kuvumilia machungu ya msiba huu mkubwa. CHADEMA tunaungana nanyi kwa moyo wa maombolezo na tunawapa pole nyingi sana kwa msiba huu mzito uliotikisa taifa.
Aidha, tunawatakia majeruhi wote uponaji wa haraka na urejeaji wa afya zao. Tunapongeza jitihada za wahudumu wa afya, pamoja na wadau wote waliosaidia katika kutoa huduma za haraka kwa waathirika wa ajali hiyo.
Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi. Amina.
Imetolewa na:
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi – Taifa
CHADEMA
08 Juni 2025
© Copyright 2025. Developed By: CHADEMA
Leave A Reply