Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antiphas Lissu, leo May 19,2025 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kesi mbili za jinai zinazomkabili
1.Uhaini
2. kuchapisha taarifa za uongo mitandaoni.
Hatua ya Lissu kufikishwa Mahakamani leo inatokana na uamuzi wa Mahakama hiyo kukubaliana na mapingamizi ya Mawakili wa utetezi kwamba Mteja wao afikishwe Mahakamani na kesi isiendeshwe kwa njia ya mtandao.
Kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa YouTube, itatajwa kwa ajili ya Serikali kumsomea hoja za awali (PH) ili kesi hiyo iweze kuendelea na usikilizwaji wa mashahidi huku kesi ya uhaini ikitarajiwa kuitishwa kwa ajili ya kutajwa.
#Stronger Together
#No Reforms No Election
© Copyright 2025. Developed By: CHADEMA
Leave A Reply