info@chadema.or.tz Daima Street, Mikocheni, Dar Es Salaam

Kuhusu Chama

KARIBU CHADEMA

Karibu CHADEMA – Chama kinachopambania Uhuru, Haki, Demokrasia na Maendeleo ya watu.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha siasa chenye misingi ya demokrasia ya kweli na maendeleo jumuishi kwa wananchi wote wa Tanzania. Kilianzishwa tarehe 28 Mei, 1992 na kupatiwa cheti cha usajili wa kudumu tarehe 21 Januari 1993, kufuatia kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania na kimejikita katika kupigania haki, usawa, utawala wa sheria, na maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi. Chama hiki kinatetea mfumo wa utawala wa majimbo wenye kutoa mamlaka zaidi kwa wananchi katika ngazi za chini, kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuzingatia mahitaji na vipaumbele vyao.

Chadema kwa Takwimu

Takwimu Tangu 1992
shap
30
Miaka ya Uhai
shap
2M+
Wanachama
shap
200+
Viongozi Kupitia Chama

Falsafa ya Chama

CHADEMA inaamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ambapo wananchi wana mamlaka ya kweli ya kuamua mustakabali wa taifa bila kuingiliwa na viongozi.

Itikadi ya Chama

CHADEMA ni chama cha mrengo wa kati kinachotetea uchumi huru na jumuishi, unaotumia rasilimali za taifa kwa manufaa ya wananchi wote.

Lengo Kuu la Chama

Lengo kuu ni kukuza demokrasia, kuimarisha maendeleo, na kuongeza uwakilishi serikalini huku likitetea muundo wa kisiasa uliogatuliwa kwa manufaa ya wananchi.

rescue man
VOLUNTEER REACH

DAWATI LA MSAADA

0793-008-292

Wasiliana Nasi
JIUNGE NA HARAKATI ZA MABADILIKO LEO!

UNGANA NA CHADEMA

Jiunge na maono yetu ya kuendeleza taifa juu

Kuwa sehemu ya harakati za kweli za demokrasia na maendeleo. Jiunge nasi leo na uwe sehemu ya mabadiliko.

Jiunge Nasi