Bavicha

Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA)

Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ni sehemu ya mabaraza ya Chama inayoundwa na Vijana wote wanachama wa CHADEMA wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 35. Pia BAVICHA linajumuisha wafuasi wa CHADEMA wasiokuwa na kadi wanaoitwa CHEMCHEM wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 17.

DIRA YA BAVICHA

ni kuona Vijana ni nguvu ya mabadiliko ya kidemokrasia kwa Maendeleo yao na ya Taifa.

DHIMA YA BAVICHA

ni kuwezesha uwepo wa sera sahihi, uongozi bora na kujenga oganaizesheni thabiti ya vijana kwa Maendeleo endelevu ya vijana wote wa Tanzania.

MISINGI YA BAVICHA

ni  Uzalendo, Uadilifu, Uwajibikaji, Umakini, Utu, Ubunifu, Umoja na Upendo.

LENGO KUU LA BAVICHA

Ili kuweza kuItimiza dhima yetu na kuifanikisha dira yetu, lengo kuu la BAVICHA litakuwa ni kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika kuwezesha Chama na Vijana kushinda Uchaguzi na kuunda Serikali.

Makala, Taarifa, Habari, Matukio ya Bavicha

Bavicha katika Picha

Share Button
Layout Settings