USAILI NA UTEUZI WA WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI ULIOFANYWA NA KAMATI KUU YA CHAMA .

Kamati Kuu ya Chama ilifanya kikao chake kuanzia tarehe 11-14 Mei,2024 kilichofanyika ofisi za Makao Makuu Mikocheni, Jijini Dar Es salaam.

1. Usaili na uteuzi wa Wagombea Kanda Nne.

Pamoja na agenda nyingine Kamati Kuu ilipata nafasi ya kuwasaili na kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Kanda nne za Magharibi, Nyasa, Serengeti na Victoria kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.

Kamati Kuu ilifanya uteuzi wa wagombea kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ibara ya 7.7.16(s) Kuteua wagombea wa Uenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Mtunza Hazina wa Kanda.

Aidha Kamati Kuu iliwaita wagombea wote waliojaza fomu Kwa mujibu wa Kanuni ya 7.2.7 ya Kanuni za Chama ”Waombaji wote wataitwa mbele ya vikao vya Uchujaji kuhojiwa na ama kutakiwa kufafanua taarifa walizozijaza katika fomu zao za maombi”.

Vilevile Kwa mujibu wa Kanuni ya 7.2.13 ya Kanuni za Chama, wagombea ambao ni wajumbe wa Kamati kuu hawakushiriki kuwahoji wagombea wenzao waliokuwa wanagombea nafasi hizo “Wajumbe wa kikao cha uchujaji ambao ni wagombea wa ngazi husika hawatashiriki katika kujadili wagombea wenzao wa nafasi hizo, lakini watashiriki katika kujadili wagombea wa nafasi zingine”.

Wagombea wote ambao hawakuteuliwa watajulishwa sababu za kutoteuliwa kwao kwa mujibu wa Kanuni ya 7.2.8 ya Kanuni za Chama “Vikao vya uteuzi vitatakiwa kuwafahamisha wale wote ambao hawatapendekezwa na kufahamishwa sababu za kutopendelezwa kwao” na wale wote ambao hawataridhika na uamuzi wa Kamati kuu wana haki ya kukata rufaa juu ya uamuzi huo Kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.

Baada ya mchakato huo wafuatao waliteuliwa na Kamati Kuu.

2. Uchaguzi wa Kanda

Baada ya wagombea kuteuliwa ratiba ya uchaguzi huo utafanyika tarehe 29 Mei,2024 katika Kanda za Magharibi, Nyasa, Serengeti na Victoria na utasimamiwa na ofisi ya Katibu Mkuu.

3. Uchaguzi wa Mkoa wa Njombe na Iringa

Kamati Kuu ilipokea na kujadili taarifa za rufaa mbalimbali ikiwemo rufaa za uchaguzi wa Mkoa wa Njombe ambao Kamati Maalum ya Kamati Kuu iliufuta uchaguzi huo kutokana na uchaguzi huo kuendeshwa bila kufuata Katiba na Kanuni za kusimamia chaguzi ndani ya Chama.

Kamati Kuu ilikubaliana na sababu za kufutwa uchaguzi huo na kuagiza ufanyike upya tarehe 25 Mei,2024 na hapatakuwa na uchukuaji wa fomu upya wala usaili bali Wagombea walewale walioshiriki duru ya kwanza ndio watakaogombea.

Aidha uchaguzi wa Mkoa wa Iringa ambao haukukamilika tarehe 09 Aprili, 2024 utafanyika tarehe 25 Mei, 2025 kwa zile nafasi ambazo hazikukamilisha uchaguzi na Wagombea walewale wa awali ndio Watakaogombea .

 

Walioteuliwa kugombea nafasi mbalimbali.

KANDA YA SERENGETI

CHAMA

UENYEKITI
1. GIMBI DOTTO MASSABA
2. LUCAS NGOTO NGOTO

UMAKAMU MWENYEKITI
1. JACKSON SCANIA LUYOMBYA

UWEKA HAZINA
1. JACKSON DAUDI TUNGU
2. KHALID SULEIMAN AUSII
3. MAENDELEO BERNARD MAKOYE
4. WILLIAM PIUS SHAYO

BARAZA LA WAZEE

UENYEKITI
1. JACOB RHOBI MONYEKA
2. SYLLVESTER MHOJA KASULUMBAYI

UKATIBU
1. CHARLES BULLET RWEGALULILA
2. KENNEDY MUSA ONYANGO

UWEKA HAZINA
1. MAGDALENA EMMANUEL MKULLA

BARAZA LA WANAWAKE

UENYEKITI
1. BAEGA STEVEN MASUNGA
2. ROSEMARY KASIMBI KIRIGINI

UKATIBU
1. ANGELA DERRICK LIMA

BARAZA LA VIJANA

UENYEKITI
1. BARAKA STEVEN CHARLES
2. MICHAEL EMMANUEL KIHANDA
3. YOHANA ZAKARIA MAGHEMBE

UKATIBU
1. PASCHAL JOSEPH MLAPA

 

KANDA YA NYASA

CHAMA

UENYEKITI
1. JOSEPH OSMOND MBILINYI
2. PETER SIMON MSIGWA

UMAKAMU MWENYEKITI
1. FRANK GEORGE MWAKAJOKA
2. JOSEPH MWASOTE MJENDA
3. MBEGESE ANOSISYE MWALUPANI

UWEKA HAZINA
1. GERTRUDA JAPHET RENGESELA
2. GRACE RICHARD SHIO
3. REHEMA PAUL MAKOGA

BARAZA LA WAZEE

UENYEKITI
1. CHARLES DAWSON NDENGA
2. HUGHO SAMALI KIMARYO

UMAKAMU MWENYEKITI
1. GERALD SIMALIKE KAJUNI
2. HENRY AMOS MHABUKA

UKATIBU
1. MPONJOLI STANELY MWAIKIMBA
2. SAADAT DAUDI MWAMBUNGU

UWEKA HAZINA
1. LYDIA DONALD MWAIPAJA

BARAZA LA WANAWAKE

UENYEKITI
1. HAPPINESS DAUDI KWILABYA
2. SUZANA CHOGISASI MGONOKULIMA
3. TABIA LUGANO MWAKIKUTI

UKATIBU
1. MARGRETH WILLIAM MLEKWA

UWEKA HAZINA
1. WITNESS MBILILILI MWANI

BARAZA LA VIJANA

UENYEKITI
1. IBRAHIM TUMAINI NYASANGA
2. VICTOR MANENO BALEKE
3. VITUS RUTINWA NKUNA

UKATIBU
1. MAGNUS FIDEL SIMBEYE

UWEKA HAZINA
1. BARAKA ABRAHAMU MWAKIHABA
2. JEREMIAH MAHASILE MNYAMBWA

 

KANDA YA MAGHARIBI

CHAMA

UENYEKITI
1. DICKSON LUCAS MATATA
2. GASTON SHUNDO GARUBINDI
3. MUSSA DANIEL MARTINE
4. NGASSA GANJA MBOJE

UMAKAMU MWENYEKITI
1. MASANJA MUSSA KATAMBI
2. RHODA EDWARD KUNCHELA

UWEKA HAZINA
1. IDAN LAURENT NDOWA
2. JOSEPHAT CLEMENT SHILOGILE
3. LAURENT MANGWESHI SENGA

BARAZA LA WAZEE

UENYEKITI
1. ADAMU KISINZA MAIGE
2. FRANCIS WILLIAM MSUKA

UMAKAMU MWENYEKITI
1. DONATUS LUPOLE KIPHUNGU

UKATIBU
1. SHABAN RAFAEL MADEDE
2. VENANCE GOMEGWA MWEMELA

BARAZA LA WANAWAKE

UENYEKITI
1. ASHURA MASHAKA MASOUD
2. MARY JAMES MARTIN
3. MONICA TARAMAEL NSARO

UMAKAMU MWENYEKITI
1. REHEMA RAFAEL MWACHA

BARAZA LA VIJANA

UENYEKITI
1. JACKSON FRANK MAULINGE
2. MOHAMED SALUM PUME

UKATIBU
1. IDRISSA KASSIM RUBIBI

UWEKA HAZINA
1. EPIPHANIA ALEX LUTEBUKA

 

KANDA YA VICTORIA

CHAMA

UENYEKITI
1. EZEKIA DIBOGO WENJE
2. JOHN JUSTINE PAMBALU

UMAKAMU MWENYEKITI
1. BAZIL JUSTINIAN WAZIRI
2. KHALID SWALEHE HUSSEIN
3. MBUTUSYO ALINANINE MWAKIHABA
4. SYLLVESTER MAGELESA MAKANYAGA

UWEKA HAZINA
1. ELIKANA PASCHAL KAHI
2. LEONARD JOSEPHAT MAGERE
3. SIJAONA JAMES KAROLI

BARAZA LA WAZEE

UENYEKITI
1. FABIAN FRANCIS MAHENGE
2. FOCUS EBIGAMBOBYENSI LAURENT

UMAKAMU MWENYEKITI
1. ALPHAXARD NYARUBWA NDIGILE
2. SHIGEMELO JAMES MAKELEMO

UKATIBU
1. GODFREY FAUSTINE MISSANA
2. LOISHIYE LAZARO TEVELI

UWEKA HAZINA
1. PHILIP MUGABU KUGURU
2. SPECIOZA STEPHANO KAMALA

BARAZA LA WANAWAKE

UENYEKITI
1. PASQUINA FERDINAND LUCAS
2. PENDO LUIS NGONYANI

UMAKAMU MWENYEKITI
1. JACQUILINY REVOCATUS KISSANGA

UKATIBU
1. DORICE NICHOLAUS MPATIL
2. ESTHER MUSA FULANO

BARAZA LA VIJANA

UENYEKITI
1. FREDY MICHAEL MASELE
2. SHABAN AVICE MABALA

UKATIBU
1. ALONI ISHENGOMA KILOMBA

Imetolewa leo Ijumaa ya tarehe 17 Mei, 2024

John Mrema

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

Share Button