1. Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu, aliyeambatana na Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, ukiingia na kupokelewa katika Uwanja wa Chipukizi, mjini Tabora baada ya kufika mkoani humo akitokea Mkoa wa Shinyanga.

2. Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu akiwasalimia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Tabora waliofika kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za mgombea huyo kwa Kanda ya Magharibi (Kigoma, Tabora na Katavi) uliofanyika katika Uwanja wa Chipukizi, mjini Tabora leo Alhamis, Septemba 3, 2020.

3. Umati wa maelfu ya wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu, kwenye Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chadema, Kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma na Katavi) uliofanyika leo Alhamis, Septemba 3, 2020, katika Uwanja wa Chipukizi, mjini Tabora.

Share Button