Picha zikionesha msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Antiphas Lissu, alipokuwa akipita maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kutokea nyumbani kwake Tegeta kuelekea Uwanja wa Tanganyika Parkers kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni, leo Jumamosi, Agosti 29, 2020. Mhe. Lissu pia alipata fursa ya kuwasalimia na kuzungumza na wananchi waliomsimamisha njiani alikopita.

Pia Picha zikionesha umati wa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakiendelea kufuatilia na kusikiliza kwa makini mkubwa mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Antiphas Lissu, katika Uwanja wa Tanganyika Parkers, Kawe, jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, Agosti 29, 2020.

Share Button