Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Goodbles Lema mamepma leo amitaka Serikali kuruhusu wachunguzi kutoka nje na kwa kufanya hivyo kutaiondolea Serikali lawama juu ya kutekwa kwa mfanjabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’
Lema aliyasema hayo leo tarehe 16 Octoba alipozungumza na mkutano wake na wanahabari Makao Makuu ya CHADEMA Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.
Mbunge huyo wa Arusha Mjini aliitaka Serikali kukubali na kuomba msaada kwenye mataifa ya nje ili waje kusaidia kufanya uchungu kutokana na matukio haya ya utekaji na kuuwawa kwa watu jambo ambao sio kama litailetea aibu Taifa kwani hata mataifa yaliyoendelea huomba msaada pale wanapopata majanga kama hayo.
“Eneo alilotekwa mfanyabiasha Mo Dewji ni eneo ambalo linaulizi mkubwa nashangazwa mpaka sasa hakuna viashiria vya kuonyesha kupatikana kwake ikiwa ni pamoja na kulinganisha juhudi za vyombo vya ulinzi na usalam kuonyesha havipo seriouse kwa jambo hili” Alisema Lema
Pamajo na kuitaka Serikali kukubali kupata msaada kutoka mataifa ya nje Mhe. Lema alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. kangi Lugola kuacha mara moja kuwazuia watu kujadili kuhusiana na kutekwa kwa mfanyabiasha Mo Dewji kwani kuwazuia ni sawa na kuwanyima watu kuli kwenye msiba.
Mfanya biashara Mo Dewji ambaye miaka mitatu iliyopita jarida la Forbes lilimtaka kuwa tajiri namba moja Afrika mwenye umri chini ya miaka 40.
Jana, familia ya Mo Dewji alitangaza zawadi kwa yeyeote yule ambaye atasaidia kufanikisha kupatikana kwa mfanyabiasha huyo zawadi ya Shilingi Billion Moja (1,000,000,000)
Mo Dewji alitekwa na watu wasiojulikana siku ya Alhamis, Oktoba 11,2018 majira ya saa 11:30 alfajiri wakati akiwa Hoteli ya Colesseum na mpaka leo tarehe 16 Oktoba saa 5:30 asubuhi hajapatikana wala kutolewa taarifa yoyoyte juu ya utekaji huo.