Mwenyekiti wa Baraza la Wanake Chadema Mhe. Halima James Mdee akiangalia kazi za mikono zinazofanywa na akina mama wajasiriamali wadogo wadogo siku ya maazimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo BAWACHA wailiazimisha kitaifa Jijini Mbeya.

 
Akiongea na akina mama mbalimbali waliojitokeza kwenye kongamano hilo Mhe. Halima Jamse Mdee aliwataka akina mama kuacha uwoga na badala yake wanatakiwa kujitokea kwa wingi ili kugombea nafasi mbalimbali za uwongozi, 
 
“Tunajua hali ya kisiasa nchini sio nzuri lakini akina mama hatupaswi kukatata tamaa na kurudi nyumba na badala yake tunatakiwa tujitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uwongozi kwenye Taifa hili ili tuweze kuleta mabadiliko” Alisema halima Mdee.
 
Share Button