KURUGENZI YA ITIKADI, MAWASILIANO NA MAMBO YA NJE

Kurugenzi Ya Itikadi, Mawasiliano Na Mambo Ya Nje

Kutokana na Maboresho mbalimbali ya kimuundo na kiutendaji ambayo chama kimeyafanya mara baada ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 , Kurugenzi ya Itifaki,Mawasiliano na Mambo ya nje iliweza kuundwa na Kamati Kuu kwa mujibu wa Katiba ya Chama ibara ya 7.7.4 na Mkurugenzi wake kuteuliwa kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 7.7.16 (b).

Kurugenzi hii iliundwa ili kuweza kutimiza malengo mapana ya chama kwa mujibu wa Mpango mkakati wa chama wa 2016-2021.

Kurugenzi hii ina idara tatu kama ifuatavyo;

  • Idara ya Uenezi
  • Idara ya mawasiliano ya Umma
  • Idara ya mambo ya Nje

Kurugenzi hii itakuwa na majukumu yafuatayo;

  1. CHADEMA Media
  2. Uenezi wa Chama
  3. Mawasiliano na umma
  4. Mahusiano na Makundi ya Kijamii
  5. Mahusiano ya Kimataifa na Diaspora
  6. Itifaki ndani ya Chama

 

Tunawakaribisha wadau wote ambao wako tayari kushirikiana nasi kama taasisi ili tuweze kuyafikia malengo tarajiwa kwa ajili ya kuwa na taifa lenye afya ya Kidemokrasia na lenye kufuata Katiba ,Sheria na kanuni tulizojiwekea.

 

Makala, Taarifa, Habari, Matukio ya Kurugenzi hii

Share Button
Layout Settings