Kesi namba 112 ya mwaka 2018 inayowakabili viongonzi wakuu na Wabunge saba wa CHADEMA imeendelea katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu leo 10/7/2018 kwa kuanza kwa kusomwa kwa mwenendo wa kesi hiyo, Hakimu anayesimamia kesi hiyo hakimu Willibard Mashauri alisoma mwenendo wa kesi hiyo.

Akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na upande wa Washtakiwa dhidi ya kutokuwa na imani na Hakimu na kumtaka ajitoe kwenye kesi, Hakimu alizipinga hoja hizo kwa kusema kuwa hazina mashiko na kukataa kujitoa huku upande wa Jamuhuri iliieleza Mahakama kuwa wao wapo tayari kwa usikilizaji wa awali wa keshi hiyo na kuiomba Mahakama kuanza kusikiliza kesi hiyo tarehe 16/7/2018 jambo ambalo lilipingwa na Wakili Msome James Mtobesya na kueleza Mahakama kuwa Sahuri la kesi hiyo limewasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaama kwaajili ya kupitiwa na kuiomba Mahakama kutopanga tarehe ya usikilizaji wa awali kutotokana na kutofahama Mahakama Kuu Kanda ya dar es Salaam utatoa uamuzi gani.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 18/7/2018 ikisubiria maamuzi na maelekezi kutoka kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Wakiwa katika chumba cha Mahakama kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo Mwenyekiti CHADEMA Taifa Mhe.Freeman Mbowe alipata nafasi ya kuzungumza na Kijana Joseph Mrunge ambaye ni mlemavu alifika mahakamani hapo kwaajili ya kufatilia mwenenda wa keshi jambo amabali lilimpelekea Mhe. Freeman Mbowe kuwaomba viongozi na wanachama mbalimbali kumchangi kijana hiyo ili kumsaidi mahitaji yake madogo madogo.

Picha ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe akiongea na Kijana Joseph Mrunge

ambaye ni mlemavu aliyehudhuria mwenendo wa kesi inayowakabili viongozi wakuu wa Chama

pamoja na baadhi ya Wabunge katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

(Picha na Abdulkarim Hussein)

Share Button