TANZIA: RATIBA YA KUAGA NA MAZIKO YA MHE.KASUKU BILAGO MBUNGE WA JIMBO LA BUYUNGU, MKOA WA KIGOMA

Tunautangazia umma kuhusu ratiba ya kuaga na mazishi ya Mbunge wa Buyungu Mhe.Kasuku Bilago ambaye pia alikuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama na Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Magharibi yenye Mikoa ya Kigoma,Katavi na Tabora.
Kwa upande wa Bunge Marehemu alikuwa Naibu Waziri Kivuli katika wizara ya Elimu na Mafunzo.

Baada ya kikao baina ya familia na Viongozi wakuu wa Chama kilichofanyika leo tarehe 27 Mei,2018 ratiba iliyokubaliwa ni kama ifuatavyo;

Jumatatu tarehe 28 Mei 2018 ni ibada fupi na kuuaga mwili katika viwanja vya Karemjee Dar kuanzia saa sita kamili mchana na mwili kupelekwa uwanja wa ndege, Dar es Salaam.

Tarehe 29 Mei siku ya Jumanne asubuhi mwili utapokelewa uwanja wa ndege, Dodoma na kupelekwa Bungeni ambapo Wabunge watauaga mwili katika viwanja vya Bunge Dodoma. Baada ya hapo mwili utasafirishwa kwa ndege kuelekea Kibondo.

Tarehe 30 Mei siku ya jumatano wananchi wa Jimbo la Buyungu watapata fursa ya kuuaga mwili katika eneo litakalotangazwa baadae.

Alhamisi tarehe 31 Mei, ndio siku ya Mazishi rasmi ambayo yatafanyika Nyumbani kwa Marehemu huko Wilayani Kakonko, Kigoma.

Kwa ratiba hii tunawatangazia rasmi wananchi wote wa Mkoa wa Dar Es Salaam kuwa kesho wajitokeze kwa wingi ili kuweza kumpa heshima za Mwisho katika ukumbi wa Karemjee .
Aidha tunatoa wito kwa Wanachama, wapenzi na Watanzania wote tuendelee kuikumbuka familia ya Marehemu katika Sala na Dua katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mpendwa wao ili Mungu aendelee kuwapa faraja.

Imetolewa na John Mrema – Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

Share Button
Layout Settings