RAIS MAGUFULI, SERIKALI YAKO IMECHAFUKA,CHUTAMA uweze KUJISITIRI!

Anaandika HALIMA MDEE (MB) : 

RAIS MAGUFULI, SERIKALI YAKO IMECHAFUKA,CHUTAMA uweze KUJISITIRI!

NDUGU RAIS naona Trillion 1.5 imekutoa mafichoni, CAG  ameivua nguo SERIKALI yako! CHUTAMA uweze kujisitiri !! USITISHE WATU!

Nasema na wewe  nikiwa nina kumbukumbu ya kukamatwa na vyombo vyako vya usalama SAA TISA ALFAJIRI (31/3/2018) na kuwekwa  ‘lock up’ kwa SIKU TATU nikiwa nimetoka kwenye MATIBABU! Naandika nikifahamu vyombo vyako vya DOLA vitakuja ‘kunikamata’ tena kwa kuwa MTUKUFU umetoa AMRI kwamba yeyote  atakayezungumzia suala la shilingi Trillion 1.5 kama lilivyoainishwa kwenye ripoti ya CAG akamatwe na afungwe!! Ngoja tuseme ili utukamate na kutufunga vizuri!!

Nimekusikia JANA kupitia vyombo vya habari ukinukuliwa ukisema  “ kuna ugonjwa tumeupata sisi watanzania wa kuamini kila kinachoandikwa  kwenye mitandao ni cha kweli,sasa sijui huu ugonjwa umetoka wapi,lakini ni kwa sababu hii itandao hatuicontrol sisi….ndio maana mkienda katika nchi kam China sina uhakika kama wana google na whatsApp kama tulizonazo sisi” mwisho wa kunukuu!! Ndugu  Rais hapa sitajadili kama CHINA  wana GOOGLE au whatsApp’  nikitambua kwamba toka umetangazwa na Tume ta Taifa ya uchaguzi kama ‘mshindi halali’ wa Urais umegoma kabisa kusafiri kwenda NJE YA  MIPAKA YA AFRIKA MASHARIKI na Kati..ukidai unaiNYOOSHA NCHI.

Kwa mantiki hiyo itakuwa vigumu sana kwako kujua kama China ‘wana GOOGLE au WHATSAPP’ Mara ya kwanza nilidhani husafiri kwa sababu ya gharama, nikaja nikagundua kwamba gharama ilikuwa ni POROJO pale ulipoamua kumtuma MAKAMU WAKO WA Rais akuwakilishe kwenye mikutano mbalimbali ya KIMATAIFA inayokutaka wewe kama MKUU wa Nchi kukutana na wakuu wa Nchi wenzako kujadili mambo MAZITO yatakayoiletea neema Nchi yetu!

Ndugu Rais natambua hasira zako dhidi ya ‘Google na whatsapp’…nadhani hapa ulikuwa una maanisha  ‘mitandao ya kijamii’! kutokana na ukweli kwamba umeshindwa kuvidhibiti kama ambavyo umefanikiwa kuvidhibiti vyombo vikuu vya habari! Huku kwenye mitandao ya kijamii watu wako huru, hawataki kulishwa matango pori ambayo wewe unatamani watanzania walishwe! Kwa lugha nyingine watanzania wanataka kujiepusha na ugonjwa  wa kuamini kila SERIKALI yako inachokisema..

Jana tumekushuhudia ukimsimamisha CAG  na kumuuliza kama kwenye ripoti yake kuna pahala ameandika kuna shilingi trillion 1.5 zilizoibiwa , kisha ukamuuliza na MTOTO wako Katibu Mkuu wa wizara ya FEDHA kama NCHI imeibiwa …. NAE akakupa jibu “hapana Mheshimiwa” ….SIJUI ULITARAJIA MTOTO atampa jibu gani BABA….

Ndugu RAIS NINA mambo 8 ambayo nataka UYASOME na kuyaelewa..KISHA utajijibu mwenyewe kama UMEFANIKIWA kuinyoosha NCHI….au NCHI Imekunyoosha….

  1. Alichokisema CAG  kwenye ukurasa wake wa 34 ,nanukuu “ Kati ya shilingi  bilioni 25,307.8 zilizokusanywa ,  shilingi bilioni  792 zilitolewa  kwa ajili  ya mishahara ya watumishi , matumizi mengine ,matumizi ya maendeleo  na fedha kwa ajili ya kulipa madeni yatokananayo  na amana za serikali  pamoja na riba’  CAG hawezi sema pesa zimeibwa au la…anachotuambia SISI wananchi ni kwamba mpaka mwaka wa fedha unaisha 30 Juni 2017. Na mpaka anawasilisha ripoti yake kwako Mwezi Machi 2018 kulikuwa kuna bakaa la shilingi Trillion 1.5 ambalo halijulikani limefanya kazi gani !Mpaka sasa si wewe wala WASAIDIZI wako walioweza kujibu ,Kwa kuwa taarifa imeshapita kwako na wewe ukatoa idhini iletwe mbele ya BUNGE, tunaomba MTUACHIE wabunge tufanye kazi yetu!! UMELIZIMA BUNGE….HUWEZI ZIMA FIKRA YAKINIFU
  1. CAG anasema nchi imeshindwa kupata mapato ya kodi  yenye thamani ya shilingi trillion 4.44 kutokana na ufanisi mdogo wa baraza la rufaa la kodi  na Mahakama ya rufaa kutokana na upungufu wa  makamu wenyeviti  na wajumbe wa  bodi zake hali inayopelekea kushindikana kufanya vikao vya kutosha hivyo serikali kukosa mapato!
  1. CAG anasema TRA haikukusanya kodi yenye thamani ya shilingi 1,827,720,075,433.35 (Trillion 1.8 ) kutokana  na mapingamizi ya kodi ambayo yalikwisha shughulikiwa  na kukamilishwa. Hivi zile ziara zako za kushtukiza na za mara kwa mara TRA  zimezaa  matunda kweli??
  1. CAG anatuambia serikali yako haifuati SHERIA  ya Manunuzi ya UMMA  na KANUNI zake wakati wa kufanya MANUNUZI, ameeleza wazi kabisa  moja ya manunuzi yaliyofanyika bila kufuata sheria ya manunuzi , ni manunuzi ya ile ndege ya Q400 BOMBANDIER yenye thamani  ya shilingi Bilioni 51.838   uliyoipigia upatu kwamba umelipa CASH  kama vile unatoa fedha zako mfukoni !SISI WAKONGWE TUNAJUA  mara nyingi DILI za NAMNA HII zina harufu za wizi na ufisadi
  1. CAG anatuambia kwamba gharama za matibabu  ya nje ya nchi katika kipindi cha MIEZI  SITA TU (30th june 2017 –Desemba 2017 ) zimeongezeka  kutoka shilingi (Bilioni 28.6  mpaka shilingi  Bilioni 45.7) Ndugu Rais ulisema kuwa katika  kipindi cha UTAWALA wako  matibabu nje ya nchi yatamalizwa kabisa/yatapunguzwa. Hata Mhe.Lissu mmegoma kumlipia MATIBABU mpaka SASA! CAG anatuonyesha kwamba umevunja rekodi kwa MATUMIZI!!  Sote tunajua hakuna anayetoka nje ya nchi ,kwa pesa ya serikali bila KIBALI CHA IKULU..’ndio maana  tulimdharau na kumpuuza waziri wako aliposema…eti wanafanya ‘uhakiki’ kwa sababu wanahisi kuna watu walidanganya wanaenda kutibiwa  moyo,lakini anakwenda kupandikizwa mimba sababu ya uzazi”
  1. CAG anatuambia kwamba SERIKALI yako ilikopa ndani zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge  kwa 10/08%.  Kitendo hiki mbali na kuwa kinyume na sheria  kina athari kubwa kwa wakopaji wengine(wafanyabiashara)kwani sehemu kubwa ya mtaji wa mabenki unakuwa umefungwa kwenye fedha  walizokopesha  Serikali  kwa muda mfupi na muda mrefu. Matokeo yake , riba ya kukopesha kwa watu binafsi  inakuwa kubwa na gharama ya maisha inakuwa juu!
  1. CAG anatuambia kwamba Serikali IMEPORA akiba za mamilioni ya WASTAAFU waliotumia jasho na damu yao kulitumikia Taifai ! IMEKOPA MIFUKO ya HIFADHI shilingi bilioni 5,343 (Trillion 5.3) na kuamrisha ilipwe shilingi bilioni 3,183 (Trillion 3.1). Serikali ituambie ,shilingi bilioni 2,160 (Trillion 2.1) ziko wapi?huu WIZI?
  1. CAG anatuambia kwamba Serikali yako ilikuwa inawadanganya watanzania kwamba TRA inakusanya mapato na kuvuka malengo !lakini tukiwaambia mtupe mchanganuo wa mapato husika , milikuwa mnapiga danadana…leo CAG amewaumbua na kutuambia kwamba mapitio ya hesabu jumuifu  yalibainisha kwamba TRA iliwadanya WATANZANIA iliposema mapato ya kodi yamefikia  kuwa shilingi 15,094,949,741,000 (Trillion 15). Ilhali ikijua kwamba Kiasi  kinajumuisha  kodi iliyokusanywa na TRA  kwa niaba ya TAASISI  nyingine shilingi 2,165,273,630,236 (Trillion 2.1).

 

Mtukufu… UNAAMINI KWELI umeinyosha NCHI? Na hapa sijazungumzika kabisa DENI la TAIFA linalolitafuna TAIFA kimya kimya…Nikuhakikishie tu, waBUNGE  , hata kama tutabaki 10 tutafanya kazi yetu ipasavyo! ….CHUTAMA….usitishe watu! HAKUNA mwenye HATIMILIKI YA Tanzania!! WATANZANIA AMKENI, USINGIZI WENU WA PONO unaligharimu TAIFA #RUDISHAPESAYETU.

HALIMA MDEE (MB)

MBUNGE – JIMBO LA KAWE

WAZIRI KIVULI : FEDHA NA MIPANGO

MWENYEKITI BAWACHA TAIFA

Share Button
Layout Settings