TAMKO: Tunalaani kwa nguvu zote udhalilishaji huu unaofanywa dhidi yetu.

Baraza la Wazee Taifa la CHADEMA lilianza ziara ya kukutana na Wazee kwenye Vikao vya Ndani jana tarehe 16.04.2018 na walianzia Mkoa wa Morogoro.    

Jambo la kusikitisha ni kuwa jana usiku Polisi walivamia walikokuwa wamelala Viongozi na kuwakamata baadhi yao ambao ni Dereva Proaches Urassa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Jimbo la Morogoro Kusini Mzee Daniel Banzi na mpaka sasa wameshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro.   

Hakuna maelezo ya maana yanayotolewa zaidi ya Polisi kusema ni ukaguzi wa kawaida, ila ukweli ni kwamba kila wanapoonekana viongozi wa CHADEMA Polisi wanawakamata.

Tunalaani kwa nguvu zote udhalilishaji huu unaofanywa dhidi ya viongozi na Wanachama wetu, dola isifikiri inaturudisha nyuma kwa matendo haya.

Imetolewa na;

John Mrema

Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

Share Button
Layout Settings