Waraka Maalum wa Mh. Freeman Aikaeli Mbowe

Leo tarehe 22 Machi 2018, mimi na viongozi wenzangu waandamizi wa Chadema tumetakiwa tena kuripoti Polisi.
Tunaokabiliwa na usumbufu huu ni pamoja na: Mhe Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Mhe. John John Mnyika, Mb na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar; Mhe Halima J. Mdee, Mb, Mwenyekiti wa Bawacha, Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. John W. Heche, Mb, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti (Mara, Simiyu na Shinyanga) na Mjumbe wa Kamati Kuu; Mhe. Esther N. Matiko,
Mb, Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Mara na Mweka hazina wa Bawacha Taifa.
Tuna taarifa pia ya kusudio la kumuunganisha Mhe. Peter Msigwa, Mb, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa) na Mjumbe wa Kamati Kuu katika shauri hili.

Soma Waraka wa Mbowe hapa

Share Button
Layout Settings