BARAZA LA WAZEE WA CHADEMA: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 7/8/2016

BARAZA LA WAZEE WA CHADEMA
TAARIFA ILIYOSOMWA MBELE YA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 7/8/2016
Ndugu wanahabari
Awali ya yote, Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), tunapenda kuwashukuru kwa kuitikia wito wetu wa kukutana nanyi.
Kupitia mkutano huu na waandishi wa habari, Baraza la Wazee CHADEMA lingependa kutumia fursa hii kusema machache kwa mstakabali wa taifa letu.
PONGEZI KWA KAMATI KUU KUAHIRISHA MIKUTANO NA MAANDAMANO YA AMANI “SEPTEMBER MOSI 2016”
Itakumbukwa kuwa Agosti 31, mwaka huu CHADEMA baada ya kupokea wito wa makundi ya watu mbalimbali katika jamii, wakiwemo viongozi wa dini, wananchi wengine mashuhuri na wenye ushawishi katika jamii, wakiwemo wazee wastaafu, kiliamua kusitisha mikutano na maandamano ambayo ilipangwa kufanyika nchi nzima, siku ya Alhamis, Septemba 1, mwaka huu.
Tunatambua ugumu ambao viongozi wakuu wa CHADEMA, kupitia Kamati Kuu ya Chama, waliupitia katika kufikia uamuzi kuahirisha ‘Septemba Mosi’, kwa namna ambavyo ari ya Watanzania ilivyokuwa juu, wakiwa wamejiandaa kufanya mikutano na maandamano kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi, kama ambavyo ilikuwa imeazimiwa na kikao maalum cha dharura cha Kamati Kuu kilichoketi Julai 23-24, jijini Dar es Salaam.
Kwa kutambua moyo wa kiuongozi waliouonyesha na dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania wote, Baraza la Wazee tunapenda kuwapongeza viongozi wetu wakuu kwa uamzi huu wa busara ambao umeuthibitishia umma wa wa Tanzania kuwa chama kina viongozi wasikivu na wavumilivu ambazo ni sifa muhimu kwa kiongozi yeyote.
Aidha, tunatumia pia nafasi hii kuwapongeza viongozi wa dini zote ambao kwa pamoja waliwaomba na kuwasihi viongozi wa CHADEMA  katika vikao kadhaa walivyofanya nao kwamba CHADEMA isogeze mbele uzinduzi wa mikutano na maandamano nchi nzima, ili waweze kufanya jitihada za kuonana na Rais John Magufuli kwa ajili ya kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa kisiasa uliopo, ili kuliepusha taifa na machafuko ya kisiasa na umwagaji wa damu ambao ungeliweza kutokea siku ya Septemba 1 kutokana na mazingira ambayo yalijengwa na viongozi wa serikali, kwa kutoa kauli za vitisho, kufanya maandalizi kutumia nguvu za kijeshi kwa kufanya mazoezi ya kijeshi mitaani wakiwa na siraha za moto.
Katika muktadha huo huo, tunapenda pia kuyapongeza makundi au taasisi zingine kama Mwalimu Nyerere Foundation, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Jukwaa la Katiba na Jukwaa la Wahariri, Mama Maria Nyerere, ambao nao kwa nafasi zao katika jamii, walitimiza wajibu wa kiuongozi, kuwasihi Viongozi wakuu wa CHADEMA, kuahirisha kwa muda mikutano na maandamano ya UKUTA ili kutoa fursa ya mazungumzo kufanyika na kupata mwafaka.
Sisi Wazee wa CHADEMA tunatambua kuwa makundi yote hayo yanajua kuwa CHADEMA walikuwa upande wa kusimamia haki inayotolewa na Katiba na Sheria za Nchi, hususan Sheria Namba 5 ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992, ambayo inaelekezautaratibu mzuri wa  namna ambavyo vyama vya siasa na wanasiasa wanapaswa kufanya siasa mahali popote katika nchi hii bila kuathiriwa na kauli za mtu yeyote.
WITO KWA MTUKUFU RAISI
Baraza la wazee CHADEMA tunatoa wito kwa mtukufu raisi kutokuupuuzia juhudi za viongozi wetu wa kiroho za kutafuta amani ndani ya taifa letu kwani jambo ili litakuwa linaendeleza utamaduniwetu mzuri wa kuwapa nafasi viongozi wetu wa dini kutumia karama zao kuleta mtengamano wa taifa.
KAULI TATA ZA MTUKUFU RAIS
Mara ya mwisho tulipokutana nanyi ndugu wanahabari, mojawapo ya mambo ambayo tulizungumzia ilikuwa ni pamoja na kile tulichokiita kuwa ni ‘kauli tata za rais’, ambapo tulisema tangu aingie madarakani Rais Magufuli amekuwa akinukuliwa akitoa kauli tata ambazo si tu zinashusha hadhi yake na taasisi ya urais, bali pia zingine zinavunja sheria za nchi waziwazi kabisa, hivyo kupelekea sintofahamu kubwa na hata sasa mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini.
Wakati ule tulitoa ushauri kuwa ni vyema Rais akawa muangalifu na kauli zake ili zisilete mapasuko katika Taifa. Lakini jambo la kusikitisha sana Rais akiwa Zanzibar katika ziara yake Tarehe 2 na 3 Mwezi alitoa matamko yanayochochea uhasama na chuki na kutishia ustawi wa umoja wa Kitaifa. Rais alisikika akiupongeza ukiukwaji wa Demokrasia uliofanyika visiwani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kudhihaki kwa kupendekeza msimamizi wa uchaguzi aliyehusika kuvuruga uchaguzi apewe tuzo na Raisi Shein.
Kwa hali ilipofikia Zanziber, Baraza la wazee CHADEMA tunashauri Rais aunde tume ya maridhiano kurejesha hali utengamano Visiwani Zanzibar badala ya kuwagawa wananchi.
NJAMA ZA KUKIFUTA CHADEMA
Ndugu wanahabari hivi karibuni tumepata taarifa kuwa viongozi wa Kamati ya uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa inayoundwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, Katibu wa Baraza ambaye ni Msajiri wa Vyama vya siasa na wenyeviti wa wa kamati nne za Baraza kuwa wamepanga njama kwa kushirikiana na serikali kuhujumu chama chetu  kwa kuandaa mitego haramu ya kisiasa ili hatimaye yatolewe mapendekezo ya kufutwa chama chetu katika Orodha ya Vyama vya Siasa.
Njama hizi zinadhihilishwa wazi na mtililiko wa matamshi ya kichokozi naya uvunjifu wa Katiba ya nchi kutoka kwa viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo waziri mkuu, wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Jeshi la polisi na Raisi mwenyewe  ya kuzuia mikutano ya kisiasa ya ndani na nje.
Si hilo tu,  Ndugu wa waandishi wa habari mtakumbuka kuwa, mnamo tarehe 15/8/2016 Wajumbe wa Kamati ya uongozi ya Baraza la uongozi ilikutana kwenye ofisi ya msajiri nakuamua kuwa kuna haja ya kuitishwa kwa kikao cha Baraza la vyama vya siasa kujadili changamoto zilizopo katika mfumo wa Demokrasia ya vyama vingi hususani zuio la mikutano ya vyama vya siasa.
Wote tulisikia kupitia vyombo vya habari kuwa kikao kilipangwa kufanyika tarehe 29 na 30 mwezi Agust 2016. Katika hali isiyo ya kawaida Kamati hii iliahirisha kikao chake nakukipeleka tarehe 3 na 4 mwezi September, 2016. Jambo ili halikutegemewa na wapenda amani kwani CHADEMA walikwishatangaza kufanya mikutano na maadamano nchi nzima siku ya tarehe 1 September, 2016 kupinga ukandamizwaji wa Demokrasia na wakati huo Raisi alikwisha kutoa amri ya watu kuvunjwa miguu iwapo watathubutu kuandamana na wakati huo jeshi la polisi likifanya mazoezi adharani kutekeleza amri ya amiri jeshi. Kwa busara ya kawaida Kamati uongozi ya Baraza la vyama vya siasa ingeliona umuhimu na uharaka wa kukaa kuepusha shari lakini kinyume chake wakatangaza kuahirisha kikao!
Jambo la kushanga zaidi baada ya busara kutumika kupitia viongozi wa dini  kushawishi CHADEMA kuahirisha kwa kutoa mwanya wa mazungumzo hadi tarehe 1 October 2016, Kamati ya uongozi ya Baraza la vyama vya siasa ikaibuka tena na kutangaza kuahirisha kikao cha baraza hadi itakapotangazwa tena. Katika mazingira haya ni nani ambaye anaweza kushida kushawishika kuwa kuwa tayari viongozi hawa wanayo agenda moja tu ya siri ambayo nikupendekeza kufutwa kwa CHADEMA mara baada ya kufanya maadamano ya kupinga ukiukwaji wa Katiba wa vyama vya siasa kufanya mikutano na maadamano ya amani.
Nimatumaini yetu kuwa njama hizi zitapingwa na watu wote wapenda amani kwani uamzi huu unaweza kusababisha machafuko makubwa nchini na kulazimisha uzalishaji wa vikundi vya kutetea demkrasia kwa njia isiyo rasimi kwani.
Si hivyo tu uamzi huu unaweza kurudisha nyuma maedeleo ya taifa kwa kulazimisha kutumia raslimali zilizoko kufanya chaguzi mbali mbali badala ya kujielekeza katika shughuli za maendeleo.

Share Button
Layout Settings